Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Athumani Msabila Mapema Leo Asubuhi August 7, 2022 ametembelea Maonesho ya Wakulima na Wafugaji (Nane Nane) na kufika banda la Manispaa hiyo katika Viwanja vya Nane Nane eneo la Ipuli Manispaa ya Tabora ikiwa ni maonesho ya Kanda ya Magharibi yanayohusisha Mkoa wa Tabora na Kigoma
Akiwa katika banda hilo amewapongeza Wajasiriamali waliojitokeza na kuthubutu kuleta bidhaa zao katika maonesho hayo kwa lengo la kutangaza Bidhaa zinazopatikana Manispaa ya Kigoma/Ujiji ikiwa ni pamoja na uuzaji wa bidhaa hizo
Katika Maonesho hayo Wajasiriamali wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji wanaendelea na kuonesha na kuuza Bidhaa kama vile Samaki wanaovuliwa Ziwa Tanganyika (Maarufu kwa jina la Mgebuka), Dagaa, Uchakataji, Usindikaji na Ufungaji wa Mafuta ya Mawese, Sanaa za Uchongaji, biashara ya Vitenge na Mashuka ya kufuma (Maarufu Mashuka ya Kigoma), Bidhaa za Viungo, na Unga wa Mhogo
Aidha Teknolojia inayoonesha katika Banda la Manispaa ya kigoma/Ujiji ni pamoja na Teknolojia ya Uzalishaji wa Miche ya Michikichi ya Kisasa aina ya Tenera, Teknolojia ya Ufugaji wa Samaki na Samaki wa Mapambo, Kilimo cha Nyanya na Mahindi
Kauli Mbiu ya Mwaka huu kwa Sikukuu ya Wakulima na Wafugaji (Nane Nane) ni " Agenda 10/30: Kilimo ni Biashara, Shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi".
Karibu Banda la Manispaa ya Kigoma/Ujiji viwanja vya Nane Nane Ipuli Manispaa ya Tabora ujipatie bidhaa na kujifunza Teknolojia Mbalimbali.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa