Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga jana Jnuari 30, alifanya ziara katika halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji kufatilia utekelezaji wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za sekondari
Ziara hiyo aliyoifanya ikiwa ni kufuatilia utekelezaji wa agizo la Ofisi ya Raisi TAMISEMI kuwa kwa halmashauri za zenye upungufu wa vyumba vya madarasa nchini kufikia februali 29, ujenzi wa vyumba vya madarsa uwe umekamilika na wanafunzi kuanza masomo yao mara moja
Katika ziara hiyo aliyoifanya akianzia katika Sekondari ya Buzebazeba , Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Ndugu. Mwailwa Pangani alitoa taarifa kuwa halmashauri ilikuwa inakabiliwa na upungufu wa vyumba vya madarsa thelathini na nane (38) , ambapo jumla ya vyumba kumi na moja (11) vipo tayari na vinaendelea kufanyiwa ukarabati ili wanafunzi kuweza kuanza masomo yao mapema mwezi march
Mkurugenzi huyo alisema vyumba vnine (4) vya madarasa vimejengwa katika shule ya sekondari Buzebazeba ambayo ni shule mpya na tayari amekwisha kupokea usajili wa shule hiyo, na madarasa mengine saba (7) yapo katika shule ya msingi Kigoma ambayo wanafunzi wamehama kutoka katika madarasa hayo na kuhamia katika madarasa mapya ambayo yameshajengwa tayari na kukamilika
Ameendelea kusema katika shule hiyo ya msingi madarasa hayo yaliyokuwa yakitumiwa na wanafunzi wa shule ya msingi yameombewa usajili ili yaweze kutumika kama shule ya sekondari na tayari wadhibiti ubora wa elimu wamekubaliana na kutoa vigezo vya shule hiyo kusajiliwa ikiwa ni pamoja na ujenzi wa ukuta au uzio wa kutenganisha shule hizo mbili ya msingi na sekonadri
Aidha ameendelea kusema madarasa hayo yaliyokuwa ya shule ya msingi yanatarajiwa kufanyiwa ukarabati na tayari kuanzia kesho fundi anatarijia kuanza ukarabati wa miundombinu hiyo ikiwa ni pamoja na ukarabati wa madarasa na miundombinu ya vyoo vya shule hiyo, na kusema shule zingine zenye upungufu wa madarasa tayari ofisi ya Mkurugenzi imenunua tofali laki nne na elfu arobaini na saba na mia tano (447500) ambapo tofali hizo zimesambazwa na zinaendelea kusambazwa katika shule ili kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa ishirini na saba (27)
Mkurugenzi huyo alihitimisha kwa kuwashukuru wananchi wa Manispaa hiyo kwa kuhamasishana kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa kutumia nguvu ya wananchi kwa hali na mali ambapo mikutano ya wananchi kwa baadhi ya kata ziliazimia kila kaya kuchangia kiasi cha Tsh 10,000/=, huku wakishirikiana na wataalamu wa kata, wenyeviti wa serikali za mitaa na wadau mbalimbali wa elimu
Naye mkuu wa mkoa akiwa katika ziara hiyo aliridhishwa na ujenzi wa shule hizo mpya za sekondari zinazojengwa huku akitoa ushauri wa kupandwa kwa miti katika sekondari ya Buzebazeba, na kuahidi kuendelea kufuatilia ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa na akiahidi kutoa mifuko ya simenti kumi (10) katika shule ya sekondari Gungu kutokana na kuridhishwa na mikakati na miundombinu ambayo imeshawekwa katika shule hiyo
Aidha mkuu huyo wa mkoa alitembelea standi ya magari makubwa ya mizigo aina ya malori inayojengwa katika halmashauri hiyo ikiwa ni agizo la mkuu huyo wa mkoa kutokana na uharibifu unaofanywa na magari hayo yanapoingia mjini kushusha mzigo huharibu kingo za barabara za mjini na kusema ujenzi wa standi hiyo itakuwa ni fursa kwa wasafirishaji wa magari madogo ya mizigo, bodabaoda, wapishi wa migahawa na nyumba za kulala wageni katika eneo hilo
Katika ziara hiyo aliyoifanya mkuu wa mkoa huyo alitembelea shule ya sekondari Buzebazeba, shule ya msingi Mnarani , shule ya msingi Buzebazeba, shule ya Sekondari Rubengera, shule ya sekondari Buronge, shule ya sekondari gungu na standi ya magari makubwa ya mizigo lililopo kata ya Gungu, ambapo pia ameongea na walimu, wanafunzi na wananchi kero zinazowakabiri katika jamii yao
Picha na matukio zaidi tembelea maktaba ya picha ya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa