Na Mwandishi wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bi. Esther Alexander Mahawe jana Desemba 15, 2021 alifanya ziara ya kutembelea ujenzi wa miundombinu ya elimu na afya unaoendelea katika Tarafa ya Kalinzi Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma huku akiwataka wasimamizi wa miradi hiyo kukamilisha kwa wakati
Mkuu huyo wa wilaya aliwataka wasimamizi ngazi ya Halmashauri, Kata, na Shule kukamilisha ujenzi huo kabla ya Desemba 30, mwaka huu huku wakizingatia thamani ya fedha kwa kila mradi unaotekelezwa
Aidha Mkuu huyo wa wilaya alisema hadi sasa ujenzi huo unaendelea vizuri kwa kuzingatia thamani ya miundombinu na itakabidhiwa kwa wakati na wanufaika kuitumia kama maelekezo yalivyotolewa kwa ngazi ya Taifa
Aliendelea kuwataka Wasimamizi hao kuzingatia mda uliowekwa huku akisema suala la usimamizi na ufatiliaji ataendelea kulifanya kila mara ili kuhakikisha miradi inakuwa katika viwango bora na kuwanufaisha wananchi wa maeneo hayo
Miradi aliyotembelea ni pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa na samani zake katika shule ya Sekondari Kalinzi kwa fedha za Kitanzania Million sitini (Tsh 60,000,000/=),ujenzi wa vyumba vitatu (03) na ukamilishaji wa maabara moja Shule ya Sekondari Mkabogo wenye jumla ya fedha za Kitanzania Million tisini (90,000,000/=) ikiwa ni fedha za Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19 na ujenzi wa vyumba vya madarasa viwili (02) Shule ya Msingi Mshikamano kwa fedha za Kitanzania Million arobaini (Tsh 40,000,000/=) kutoka kwa mradi wa EP4R
Miradi ya idara ya Afya aliyoitembelea ni pamoja na ujenzi wa kituo cha afya kijiji cha Mlangala kwa fedha za kitanzania Million mia mbili hamsini (Tsh 250,000,000/=), ujenzi wa wodi ya wazazi na matundu matano (05) ya vyoo Zahanati ya Kijiji cha Kalinzi ikiwa ni fedha kutoka Serikali Kuu
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa