Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bi. Ester Alexander Mahawe amezitaka Taasisi na Idara za Serikali kusimamia fedha za miradi zinazoletwa wilayani hapo zitumike kwa usahihi pasipo kuwa na ubadhilifu
Ameyasema hayo leo October 11, 2021 wakati akifungua Mkutano wa wadau wa Maji Manispaa ya Kigoma/Ujiji chini ya mradi wa uwazi na uwajibikaji katika sekta ya maji unaofadhiliwa na Asasi ya Nyakitoto Youth For Development Tanzania(NYDT) uliofanyika katika ukumbi wa Hotel ya Just in Time
Amesema amemuelekeza Katibu Tawala wa Wilaya kuwaandikia Taasisi na Idara zote za Serikali kupeleka taarifa ya fedha zote za miradi zilizopokelewa kutoka Serikalini na Wadau wengine wa Maendeleo kwa lengo la kuzimamia na kuhakikisha miradi iliyokusudia inatekelezwa kwa manufaa ya wananchi
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya amesema kwa sasa ujenzi wa mradi wa Maji unaendelea kujengwa ukiwa na uwezo wa Kuzalisha lita za maji Million mia moja na arobaini na Mbili (lita 142,000,000) na Matumizi yakiwa Lita Million mia moja ishirini na tatu (lita 123,000,000) kwa wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji ambapo tatizo la kukatika kwa Maji litakuwa limekwisha na maji mengine kutumika katika Vitongoji na Vijiji vya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma
Mkuu huyo wa Wilaya amekemea vitendo vya baadhi ya watumishi wa idara ya maji wasiokuwa waaminifu kuomba Rushwa kwa wateja wanaoenda kupata huduma ya kufungiwa maji majumbani na wengine kuwabambikizia wananchi malipo (Bill) kubwa kwa lengo la kujinufaisha huku akisema vitendo hivyo hatavifumbia macho pindi anapopata taarifa zilizo sahihi
Ameendelea kusema mradi huo tayari umeanza kufanya kazi na wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji na wakazi wa Mji mdogo Mwandinga wameendelea kunufaika huku akisema tayari mkandarasi anaendelea kujenga kwa kipindi cha mwaka mmoja kutokana na Mkandarasi wa awali kushindwa kukamilisha ujenzi huo
Mkuu huyo wa Wilaya ametoa agizo la kutaka kuzifahamu Asasi zote zisizo za Serikali (NGO’s) zinazofanya kazi katika wilaya hiyo kwa lengo la kutambua shughuli na miradi inayotekelezwa kwa ajili ya kuwasaidia na kuwainua Wananchi wa Wilaya hiyo huku akiipongeza asasi ya NYDT kwa uwazi na uwajibikaji wao
Diwani wa kata ya Mwanga Kaskazini Mhe. Sharon Mashanya amesema kikao hicho kinatarajia kuleta tija kwa Wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji ya upatikanaji wa maji kutokana na ufatiliaji utakaokuwa ukifanyika kuanzia kamati za maji zilizoundwa na wananchi ngazi za mitaa
Meneja mradi wa uwazi na uwajibikaji katika sekta ya Maji kutoka asasi ya Nyakitoto Youth For Development Tanzania Ndugu. Ramadhani Joel amesema Mkutano huo wa wadau wa Sekta ya Maji umewakutanisha kwa lengo la kujadili Fursa, changamoto na Mafaniko ya upatikanaji wa Maji katika Kata tisa za Manispaa hiyo mbapo mradi huo unatekelezwa
Mkutano huo umehudhuliwa na Wataalamu kutoka KUWASA, Ewura CCC, TANESCO, TAKUKURU, Madiwani, na kamati za Wananchi za Maji ngazi ya kata ambazo zimeweza kuunda kamati ndogo za ufatiliaji wa upatikanaji wa maji
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa