Na Mwandishi wetu
Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Kigoma ikiongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo Bi. Ester Mahawe leo Septemba 8, 2021 imefanya ziara na kukutana na wananchi ambao ni wahanga wa bwawa la Katubuka liliojaa maji na kuathiri Makazi yao
Mkuu huyo wa wilaya ya Kigoma amewashauri wahanga hao kuondoka katika eneo hilo kabla ya athari kubwa kuelekea kipindi cha mvua na kutafuta maeneo mengine huku akisema anaenda kukutana na wataalamu kuona namna gani ya kuwasaidia wananchi wa eneo hilo ili kuepukana na maafa yanayoweza jitokeza
Kaimu Mkuu wa idara ya Mipango miji, Ardhi na Maliasili Ndugu. Steven Ambrose amesema katika kipindi cha miaka ya nyuma (1990s) idara ya ardhi Mkoa wa Kigoma ilipima viwanja katika eneo hilo na kugawiwa kwa wananchi na baadae eneo hilo kuanza kujaa maji huku mwaka 1995s Wakazi wa eneo hilo wakipewa fidia na kutakiwa kuhama licha ya wengine kukaidi agizo hilo na kuanza kuuza viwanja kwa watu wengine ambao ni waathirika kwa sasa
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwanga ambapo bwawa hilo linapatikana Ndugu. Mfaume Kimeya amesema historia inaonesha kuwa eneo hilo limekuwa likijaa na kukauka mara kwa mara katika kipindi cha miaka ya 1990 hadi 1997 huku baadhi ya wananchi wakifanya makazi katika eneo hilo kutokana na kupungua na kukauka kwa maji na wengine kwa kuuziwa kama viwanja vya makazi bila kujua historia ya eneo hilo
Ameendelea kusema eneo hilo limekuwa likitumika kwa kilimo cha bustani na ufugaji kwa kipindi cha mda mrefu huku akiitaka Serikali ione namna ya kuwasaidia Wananchi ambao ni wahanga na waathirika wa eneo hilo kwa kuwasaidia kupata viwanja vingine
Mmoja wa wahanga na mkazi wa eneo hilo Ndugu. Steven Mgalu amempongeza Mkuu wa wilaya kufika katika eneo hilo na kuonana na wahanga wa bwawa hilo na kuitaka Serikali kuandaa mkakati wa kuwasaidia wananchi wa eneo hilo kuepukana na athari za bwawa hilo
Bwawa la Katubuka lipo katika Kata ya Katubuka lililopo Manispaa ya Kigoma/Ujiji likikadiriwa kuwa na Viwanja hamsini na nne (54) huku baadhi ya wakazi wa jirani na eneo hilo wakisema katika kipindi cha miaka ya 1989s eneo hilo lilikuwa likijaa maji na kulazimika wakazi na wanachi kutumia mitubwi kuvuka kwenda upande mwingine
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa