Na mwandishi wetu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Suleimani Jafo leo june 4, amefanya uzinduzi wa barabara nane(8) zenye urefu wa Km 12.032 zilizojengwa kwa gharama ya Bilion 19.64 kwa ufadhili wa Benki ya Dunia (WB) chini ya Mradi wa Uendelezaji wa Miji na Majiji Kimkakati Tanzania(TSCP)
Kabla ya uzinduzi huo ametembelea barabara hizo nane na mifereji ya maji ya mvua iliyojengwa katika mradi huo yenye urefu wa Km 2.35 mfereji wa Katonyanga na mfereji wa Mlole
Waziri huyo ameongea na wananchi katika eneo la Mwembetogwa ambapo ndipo jiwe la uzinduzi wa mradi huo limewekwa kando ya barabara iliyojengwa ya Mwembetogwa-Kitambwe hadi Mwanga
Akiwahutubia wananchi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji amesema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dr. John Pombe Magufuli imejipambanua katika kuwatumikia wananchi na kuhakikisha maendeleo yanapatikana
Amesema Serikali ilipokea zaidi ya Billion mia nane(800) kutoka Benki ya Dunia(WB) ambapo ilielekeza katika Halmashauri nane(8) ili kukuzaji miji na Majiji, ambapo Manispaa ya Kigoma/ujiji nayo ilipokea fedha za ujenzi wa miradi hiyo ya barabara, mifereji ya Maji, ujenzi na ununuzi wa mitambo ya uendeshaji wa Dampo
Waziri Jafo ameendelea kusema “watu wa Kigoma nimeridhika na ujenzi wa barabara hizi, mmesimamia vizuri na miradi hii iko chini yangu, hivyo niwambie barabara hizi mnazoziona ni maelekezo ya Mhe. Rais na amenituma nihakikishe kuona barabara hizi zinakuwa katika viwango vinavyotakiwa , hivyo niwambie kiukweli nimeridhika na miradi hiyo na niwatake muweze kuitunza”
Waziri huyo amehitimisha kwa kuwataka wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa kuendelea kuchukua hatua stahiki za kujikinga na ugonjwa wa #covid-19 kwa kupiga nyungu mara kwa mara na kuendelea Kumuomba Mungu huku akisema hata Watarii nao wanaoingia Nchini wanapiga nyungu kama sehemu ya utalii na kujikinga na ugonjwa huo
Naye Mkuu wa Mkoa Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga amewataka wakazi wa Manispaa hiyo kutunza barabara hizo na kuhakikisha wanaboresha makazi yao ya kuishi kwa kuboresha nyumba zao hasa wale waliopitiwa na barabara katika makazi yao
Akisoma taarifa ya mradi huo Mhandisi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Eng. Wilfred Shimba amesema katika ujenzi wa mradi huo Kiasi cha Tsh Billion 1.10 kilibaki(Saving) na kuongeza kazi za ujenzi wa vipande vya barabara vyenye Km 0.75 ambavyo vinaingia katika barabara kuu
Mhandisi huyo amesema Manispaa ya Kigoma/Ujiji ni moja kati ya Halmashauri nane(8) zinazotekeleza mradi wa Serikali ya Tanzania kupitia mkopo wa Benki ya Dunia, ambapo Halmashauri zingine ni Majiji ya Arusha, Tanga, Mwanza, Mbeya,Dodoma na Manispaa za Ilemela, Mtwara Mikindani na Kigoma/Ujiji
Mhandisi huyo amehitimisha kwa kusema Manispaa ya Kigoma/Ujiji kupitia wataalamu wake kwa kushirikiana na Wananchi watahakikisha wanasimamia miundombinu ili kuitunza na kutoharibiwa na watu wenye nia ovu
Barabara zilizojengwa Manispaa ya Kigoma/Ujiji ni Barabara ya Kaaya-Simu, Mwanga-Kitambwe-Mwembetogwa, Barabara ya Kakolwa, Ujenzi-Nazarethi, Kagashe, Wafipa-Kagera, Maweni-Burega na barabara ya kuingia Hospitali ya Mkoa (Hospitali ya Maweni kwa Kiwango cha Lami, Ujenzi wa mifereji ya mvua ya Mlole na Katonyanga pia ujenzi wa miundombinu ya kutupia taka(skip pads)
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa