Na Mwandishi wetu
Mradi wa USAID Kizazi kipya Jana August 18, 2021 ulipongezwa na wadau mbalimbali ikiwemo wanufaika wa mradi huo Mkoani Kigoma
Pongezi hizo zilitolewa katika tukio la Kufunga mradi wa USAID kizazi kipya kwa ngazi ya Mkoa lililofanyika katika Ukumbi wa Hotel ya Sunset iliyopo Manispaa ya Kigoma/Ujiji
Mgeni Rasmi katika tukio hilo Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa Dr. Godfrey Smart aliishukuru taasisi ya BAKAIDS kwa kusimamia mradi huo wa Kizazi kipya kwa kutoa huduma za Afya na UKIMWI, ulinzi na Usalama wa Mtoto na ukuzaji wa kaya Kiuchumi
Pia Mgeni Rasmi aliwapongeza wafadhili wa Mradi huo kwa kutoa fedha zao katika kuboresha na kukuimarisha nyanja mbalimbali za Maisha ya wakazi wa Mkoa wa Kigoma huku akiwataka kushirikiana na Serikali katika Kuimarisha elimu ya Lishe na Kutokomeza ugonjwa wa Malaria Mkoani hapo
Akitoa taarifa ya shughuli zilizotekelezwa na mradi kwa kipindi cha Miaka minne (2018-2021) Afisa Afya na Ukimwi BAKAIDS Ndugu. Hamisi Karisha alisema mradi umekuwa ukiwafikia watoto na wazazi wanaoishi na Ukimwi , kupunguza umasikini miongoni mwa Wahitaji na kuongeza uelewa juu ya haki za watoto na kupinga ukatili wa Kijinsia
Alisema kwa Mkoa wa Kigoma awali Mradi wa USAID Kizazi kipya ulifadhiliwa kwa Halmashauri ya Kibondo, Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji na Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza, na baadae Halmashauri ya Kibondo kuondolewa katika mradi huo
Akitoa takwimu alisema mradi Umefanikiwa kuwafikia Wanufaika elfu saba mia nane ishirini na mbili (7,822) kwa Halmashauri ya mbili ambapo Bima ya afya kwa kaya elfu moja mia tatu hamsini na moja (1,351) na kuwafikia walengwa elfu nne mia tatu themanini na nane (4,388), mafunzo ya ufundi stadi yakitolewa kwa vijana watano (05) na wanafunzi mia mbili kumi na sita (216) wakipatiwa vifaa vya shule
Diwani wa Kata ya Kitongoni Manispaa ya Kigoma/Ujiji Mhe. Himidi Omary alipongeza mradi wa USAID Kizazi kipya kwa namna walivyokuza uchumi kwa kutoa fedha na vifaa vya kazi kwa vijana na makundi mbalimbali ya waathirika wa Virusi vya Ukimwi na kusema wao kama wawakilishi wa wananchi watahakikisha wanafatilia maendeleo ya walionufaika na mradi huo
Diwani huyo aliwataka viongozi wa BAKAIDS kusajiri vikundi walivyokuwa wakihudumia ngazi ya Halmashauri ili vipate sifa ya kuhudumiwa Mikopo ya Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu ambapo Manispaa ya Kigoma/Ujiji ilikuwa na vikundi vya wajasiriamali
Thelathini na saba (37) vikiwa na wanachama mia nne thelathini na tisa (439) na Uvinza wakiwa na vikundi 10 vyenye wanachama mia mbili kumi na tisa (219) katika mradi wa USAID Kizazi kipya
Mmoja wa wanufaika wa Mradi wa USAID Kizazi kipya Mkazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Revina Mabuga alisema yeye ni mwanachama katika kikundi cha wajasiriamali kilichokuwa kikifadhiriwa na mradi huo na wao kama wanachama wameweza kupata mafunzo na semina mbalimbali za umufamaji mashuka, kilimo cha bustani na utengenezaji sabuni jambo ambalo limekuza uchumi wao
USAID Kizazi kipya ni mradi uliokuwa chini ya asasi ya kiraia BAKAIDS ukifadhiriwa na Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa kupambana na UKIMWI (PEPFAR) na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) ambapo Nchini Tanzania ulianza rasmi mwaka 2016
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa