Na Mwandishi Wetu
Mbio za Mwenge wa Uhuru Manispaa ya Kigoma/Ujiji zimeridhia miradi ya maendeleo Saba (07) kwa kuweka mawe ya Msingi, kuzindua, kutembelea na kukagua miradi yenye yenye thamani ya fedha za Kitanzania 48,914,627,659.80.
Akizungumza katika miradi ya Maendeleo Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu. Ismail Ali Ussi amesema Serikali imeendelea kusogeza huduma karibu na Wananchi kwa kujenga miundombinu mbalimbali.
Aidha amewataka Wananchi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji kujitokeza kupiga Kura katika Uchaguzi Mkuu utaokafanyika Octoba 29, Mwaka huu.
Mwenge wa Uhuru umekagua na kuweka jiwe la Msingi ujenzi wa bweni la Wanafunzi Shule ya Sekondari Buronge kwa gharama ya Tsh 136,000,000/=, kukagua Shughuli za Vijana na kukabidhi hundi ya Mkopo wa asilimia 10% kwa Kikundi cha Vijana wa Umoja mafundi Seremala Katubuka kiasi cha Tsh 20,000,000/=, kutembelea na kukagua shughuli za lishe, UKIMWI, Malaria, Ustawi wa jamii, msaada wa Kisheria na Matumizi ya nishati Safi ya kupikia.
Aidha miradi mingine ni kukagua na Kuzindua Ofisi ya Kata ya Kasimbu iliyojengwa kwa Mapato ya ndani kwa gharama ya fedha za Kitanzania Tsh 64, 446,400/=, kuweka jiwe la Msingi Ujenzi wa Zahanati Kata ya Rubuga kwa gharama ya159,055,493.00 hadi kukamilika, Kukagua na kuzindua Barabara ya Met, kutembelea na kukagua shughuli za uhifadhi wa chanzo maji cha Amani Beach na kuweka jiwe la Msingi katika Ujenzi wa Hotel ya Kg one.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa