Na Mwandishi Wetu
Mwenge wa Uhuru Manispaa ya Kigoma/Ujiji umepitia na kuridhia kwa kukagua, kuzindua na kuweka jiwe la Msingi katika miradi kumi na mbili (12) yenye thamani ya fedha za Kitanzania zaidi ya Billion tatu ( Tsh 3,075, 506, 668.70/=)
Kiongozi wa Wakimbiza Mwenge Kitaifa Ndugu. Abdalla Shaib Kaim akizungumza mara baada ya kukamilika kwa miradi yote amesema wameridhishwa na miradi iliyokagualiwa, kutembelewa na kuzinduliwa
Mwenge wa Uhuru Umeweka jiwe la Msingi Ofisi ya Kata Buhanda, Jiwe la Msingi Zahanati ya Machinjioni, Kuzindua barabara ya Kiwango cha lami Meti, Uzinduzi wa Vyumba vya madarasa Shule ya Msingi Katubuka, Uzinduzi wa Ofisi ya Kata ya Katubuka, Kukagua shughuli za kikundi cha Azanua Vijana Kazi,, kukagua shughuli za Lishe na kutembelea Shamba la bustani ya mbogamboga Shule ya Sekondari Kigoma, na kuweka Jiwe la Msingi Tenki la Maji Kamala
Aidha Mwenge wa Uhuru Umekagua Shughuli za kupinga dawa za kulevya Shule ya Sekondari Kigoma, Kukagua Shughuli za klabu ya kupinga na kupambana na Maambukizi ya VVU/UKIMWI, na Kukagua shughuli za Kupinga Rushwa Shule ya Msingi Katubuka
Kauli mbiu ya Mwaka huu ni "Tunza mazingira, Okoa vyanzo vya maji kwa ustawi wa viumbe hai, na Uchumi wa Taifa"
Kupata taarifa nyingi zaidi endelea kutembelea www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa