Halmashauri ya manispaa ya Kigoma/Ujiji imetenga zahanati ya Bangwe ikiwa ni maandalizi ya kuwahudumia wagonjwa wa Ebola endapo watabainika kuwepo katika manispaa hiyo ikiwa ni tamko la wizara ya afya, jinsia wazee na watoto .
Yamebainishwa leo octoba 1, kamati ya Uchumi,Elimu na Afya ilipokuwa katika ziara yake ya siku mbili ya kutembelea miradi mbalimbali ikiwemo vituo vya afya na elimu(shule), akitoa taarifa hiyo Mganga Mkuu wa manispaa hiyo Dr.Siwale amesema tayari eneo hilo limetengwa kwa ajili ya shughuli ya kuwahudumia wagonjwa wa Ebola endapo watabainika kuwepo katika manispaa hiyo.
Ameendelea kusema hadi sasa hakuna mgonjwa ambaye amegunduliwa kuwa na dalili za ugonjwa wa Ebola katika manispaa hiyo na tayari wataalamu afya wameshapatiwa elimu na vifaa ni namna gani wanaweza kuwahudumia wagonjwa .
Ameendelea kusema hadi sasa wataalamu watano (5) kutoka wizara ya afya, jinsia, wazee na watoto wapo katika manispaa hiyo kwa ajili ya kutoa elimu kwa wataalamu wa afya, na na kwa wananchi, ambapo amesema wananchi wanaendelea kupata elimu katika mikutano ya hadhala anayoifanya mkuu wa mkoa wa Kigoma na mkuu wa wilaya hiyo.
“Wananchi wataendelea kupata elimu kupitia mikutano hiyo na tayari tumeandaa utaratibu wa kuwafikia wananchi moja kwa moja kupitia mikutano ikiwa elimu ya ugonjwa wa Ebola ni agenda kuu na kupitia vyombo vya habari tulivyonavyo” amesema Dr. Siwale
Amehitimisha kwa kusema wagonjwa waliokuwa wakitibiwa katika zahanati ya Bangwe watakuwa wakitibiwa katika zahanati ya Kigoma mjini ili kupisha huduma itakayokuwa ikilotewa hapo na hadi sasa maandalizi yamekamilika ambapo pia eneo la zahanati ya Bangwe inatarajiwa kuwekewa uzio kwa ajili ya usalama.
Naye mwenyekiti wa kamati ya uchumi, elimu na afya Mhe. Hussein Kaliyango ameipongeza serikali na mganga mkuu wa manispaa kwa jitihada wanazozifanya katika kuhakikisha wanadhibiti na kutoa elimu ya ugonjwa wa Ebola kwa wakazi wa manispaa ya Kigoma/Ujiji na kuwataka wakazi wa Bangwe kuitikia vizuri suala la kutibiwa katika kituo cha zahanati ya Kigoma mjini pindi watakapotangaziwa kutokana na huduma itakayotolewa.
Shirika la afya duniani WHO na Wizara ya afya , jinsia, wazee na watoto imethibitisha kuwa hadi sasa Ugonjwa wa Ebola haupo nchini Tanzania , 'Hakuna taarifa zilizopo kuhusu vipimo vya maabara na matokeo ya vipimo wala maelezo kuhusu dalili'', limesema shirika hilo la Afya duniani katika ripoti yake.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa