Na Mwandishi Wetu
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara Mhe. Christina Mndema Leo August 05, 2022 amefanya ziara ya kukagua Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari unaoendelea kata ya Businde
Akiwa katika Ujenzi wa Shule hiyo Mpya ameipongeza Serikali ya Awamu ya sita kwa Ujenzi wa Mradi huo kutokana na eneo hilo kutokuwa na Shule ya Sekondari hapo awali
Amewataka viongozi wa Manispaa hiyo kuanza Ujenzi wa mabweni, madarasa ya kidato cha tano na sita, Nyumba za Walimu kwa kutumia nguvu za Wananchi pamoja na mapato ya ndani
Ameendelea kuwataka Viongozi wa Halmashauri na taasisi za Serikali Nchini kupima maeneo ya Umma na kupata hati miliki ili kuepusha migogoro na wavamizi wa kujenga maeneo ya Umma
Amewasihi Wananchi wa Kata ya Businde kulinda na kutunza Miundombinu hiyo ya shule kwa lengo la kunufaisha Wanafunzi wa Kitanzania walio wengi
Amehitimisha kwa kuwataka Wananchi Wote katika Manispaa hiyo kujitokeza katika zoezi la Sensa ya Watu na makazi inayotarajia kufanyika Agost 23, Mwaka huu ili Serikali kuendelea kupanga Mipango na Miradi mbalimbali ya Maendeleo kwa manufaa ya Wananchi
Awali Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Athumani Msabila amesema Manispaa hiyo ilipokea kiasi cha fedha za Kitanzania Million Mia nne sabini (Tsh 470,000,000/=) kwa ajili ya Ujenzi wa vyumba vya Madarasa nane (08), Chumba kimoja cha Tehama, Maktaba, Jengo la Utawala, Matundu ya vyoo ishirini (20), Miundombinu ya Maji na ya kunawia mikono
Mkurugenzi huyo amesema kwa Sasa Ujenzi huo upo hatua ya Usafi huku akiomba Serikali kuu kuendelea kuleta fedha kiasi cha Tsh Millioni Mia moja thelathini (130,000,000/=) kwa lengo la kukamilisha Ujenzi wa nyumba za Walimu
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa