Naibu meya manispaa ya Kigoma Ujiji mhe. Athuman Juma Athuman jana septemba 19, amekabidhiwa kisima kilichojengwa na African Muslim Agency kilichojengwa katika kata ya Kitongoni katika eneo la machinjio ya nyama na kusema machinjio hayo ni ya kizamani yataendelea kuboresha.
Katika hafla hiyo ya makabidhiano iliyofanyika majira ya asubuhi akiwahutubia wananchi waliofika katika eneo hilo la machinjio naibu meya huyo aliwashukuru wafadhili hao kwa kujenga kisima hicho cha maji na kusema ni fursa nzuri kwa wachinjanji katika kutumia maji hayo lakini pia fursa kwa wafanyabiashara wa vyakula katika eneo hilo katika kuboresha afya za walaji, wauzaji wenyewe ili kuweza kuepuka magonjwa kama ya mlipuko.
Aliendelea kuwataka wafadhili hao kuendelea kujenga visima hivyo pale wanapokuwa wameombwa kufanya hivo kwani itafanya kupunguza tatizo la maji kwa Manispaa ya Kigoma Ujiji na naibu meya huyo aliendelea kuwataka wakazi wanaozunguka eneo hilo kutunza kisima hicho katika matumizi yake ili kiweze kuendelea kuwanufaisha wananchi wa eneo hilo ,wafanyabiashara na wachinjanji wa eneo hilo.
Naye Afisa Utumishi Berneth Ninalwo aliyehudhulia katika hafla hiyo ya makabidhiano kwa niaba ya mkurugenzi aliwashukuru wafadhili wa ujenzi huo wa kisima ambacho kitakuwa msaada mkubwa kwa wananchi, lakin pia aliendelea kuwashukuru wananchi, wafanyabiashara wa vyakula na wachinjaji kwa kujitokeza kwa kiasi kikubwa katika makabidhiano ya kisima hicho.
Aliendelea kusema ofsi ya mkurugenzi bado inafursa kubwa wa kuendelea kutafuta wafadhili wengine kwa lengo la kuboresha machinjio hayo na kuwa ya kisasa zaidi na kusema “kwa sasa tumeanza na upatikanaji wa maji hatua inayofuata tunajenga bafu nzuri na bora ili wachinjaji wanaofanya shuguli zao hapa, wanapomaliza watoke hapa wakiwa safi wakiwemo na akina mama wanaouza vyakula eneo hili.”
Naye mwakilishi kutoka kampuni ya African Muslim Agency wafadhili wa kisima hicho ameshukuru uongozi wa halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji chini ya mkurugenzi kwa ombi walilopewa la ujenzi wa kisima hicho, na kusema tayari katika manispaa hiyo wameshajengwa visima vya kutosha katika kata tofauti tofauti na kuendelea kuahidi kuwa wataendelea kufanya hivyo kadri ya mahitaji ya wakazi hao.
Aliendelea kuwataka halmashauri kupitia serikali ya mtaa iliyokabidhiwa kukitunza kwa maslahi ya umma kwani maji ni sehemu muhimu ya maisha ya binadamu,
Nao baadhi ya wananchi waliofika eneo hilo wameshukuru wafadhili hao kwa ujenzi wa kisima hicho na kusema maji hayo yatawanufaisha kwa kiasi kikubwa.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa