Naibu meya manispaa ya Kigoma/Ujiji Mhe. Athumani Mussa Athumani leo july 25, awaaga wakuu wa idara (wataalamu) wa halmashauri kwa safari ya kwenda ibada ya Hija nchini Saudi Arabia.
Katika mkutano huo aliofanyika ukumbi wa halmashauri hiyo naibu meya alianza kwa kuwashukuru wakuu wa idara hao kwa mwitikio wao wa kuingia kumusikiliza, ambapo aliendelea kusema ameweza kupata ufadhili ambao alikuwa hautarajii wa kwenda katika ibada hiyo ya hija .
Amemtaka mkurugenzi , wataalamu na madiwani kuwa na mahusiano mazuri katika utendaji wa kazi wao na kuondoa tofauti zilizopo kitu ambacho ndio msingi na kusema halmashauri anaiacha katika hali shwali na angependa aikute ikiwa shwali pia ambapo atakapo kuwa hija atakuwa akiendelea kuliombea swala hilo .
Ameendelea kumtaka mkurugenzi wa halmashauri kupitia wataalamu alionao kuweka mikakati imara ya ukusanyaji mapato kwa lengo la kuikuza halmashauri kiuchumi, kuweka mikakati mizuri ya kufanya usafi ikiwa ni pamoja na kufanyika kwa vikao vya mara kwa mara.
Naye mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji Dr. John Shauri Tlatlaa amempongeza naibu meya huyo kwa safari yake ya kiibada na kumpongeza kwa hatua aliyoifanya ya kuwaaga wataalamu na Manispaa kwani ni wachache ambao huaga katika safari zao wanazozifanya.
Mkurugenzi aliendelea kumpongeza naibu meya huyo kwa kutaka kuleta mahusiano mazuri baina ya wataalamu pamoja na madiwani jambo lililokuwa linaleta dalili za kuvunjika kwa mahusiano yao ya awali na kuendelea kusema ushauri mwingine alioutoa naibu meya huyo kama mkurugenzi ataufanyia kazi na kuweza kuusimamia.
Nao wakuu wa idara waliweza kupata fursa ya kumuaga mmoja mmoja ambapo wengi wao akiwemo Afisa utumishi Berneth Ninalwo ambapo walimpongeza kwa ibada ya hija anayoende kutekeleza ikiwa ni miongoni mwa nguzo 5 za ibada katika dini ya Kiislamu ulimwenguni pote na walimtakia safari njema katika ibada hiyo itakayofanyika huko Saudi Arabia, na kumtaka aiombee halmashauri na uongozi uliopo, na kuombea wakazi wote wa halmashauri ya manispaa ya Kigoma Ujiji.
Ibada ya hija ni ibada ambayo huwa inafanyika katika miji mitakatifu ya kiislamu ya Makka na Madina nchini Saudi Arabia ambapo mapema mwaka huu mfuti mkuu wa Tanzania aliwataka watanzania kujitokeza kwa wingi katika kutimiza nguzo hiyo muhimu ya dini ya kiislamu ambapo hadi hivi sasa suala la malazi, huduma za afya na chakula zimehakikishwa kuwa katika mazingira mazuri nchini huko.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa