Na Mwandishi Wetu
Watumishi wa Umma Wilaya ya Kigoma wametakiwa kufanya kazi kwa weredi katika maeneo yao ya kazi ikiwa ni pamoja na kutoa huduma bora kwa Wananchi kwa kuzingatia utaratibu, kanuni na sheria
Aliyasema hayo Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe. Deogratius Ndejembe jana Novemba 14, 2022 Wakati akizungumza na watumishi wa Wilaya hiyo katika Ukumbi wa Redcross Manispaa ya Kigoma/Ujiji
Akiwa katika ukumbi huo aliwataka Waajiri katika maeneo yao kutenda haki kwa watumishi ikawa ni pamoja na Uandaaji, uhakiki na uwasilishaji kwa wakati madeni ya Watumishi wanaodai ili kushughulikiwa kwa wakati katika wizara hiyo
Aidha aliwataka Waajiri kujiridhisha kukidhi vigezo kwa Watumishi wanaoomba kuhamia maeneo mengine ya kazi kwa kuwatendea haki huku akiwataka kuchukua hatua za kinidhamu kwa Watumishi wanaotumia nyaraka za kugushi kutaka kuhamia vituo vingine
Alihitimisha kwa kusema Serikali inaendelea kuboresha maslahi ya Watumishi Umma katika kipindi cha awamu ya sita huku akiendelea kusisitiza Waajiri kulipa stahiki za Watumishi zitokanazo na mapato ya ndani kwa wakati kama vile fedha za matibabu
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kigoma ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bi. Ester Alexander Mahawe aliwataka Waajiri wa Mkoa huo kuhakikisha wanatenda haki na kuahidi kuendelea kusimamia weredi wa watumishi kupitia Maafisa utumishi waliopo katika taasisi zao
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Athumani Msabila alimuomba Naibu Waziri h kufanya msawazo wa watumishi kutoka maeneo mengine kutokana na Halmashauri zilizopo Mkoani Kigoma kuwa na uhaba wa watumishi huku kiongozi akiahidi kulifanyia kazi
Mkutano huo ulihudhuriwa na Watumishi wa Sekratieti ya Mkoa, Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji, Halmashauri ya Wilaya na Watumishi kutoka taasisi na idara za Serikali Wilaya ya Kigoma
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa