Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Kisena Mabuba amesema ndani ya Siku 100 za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dr. Samia Suluhu Hassan tayari inatekeleza kuanza kwa ujenzi wa Soko la kisasa katika Mwalo wa Kibirizi.
Ameyasema hayo Leo Novemba 25, 2025 katika kipindi cha #GoodmorningKigoma kinachorushwa na Radio Joy iliyopo katika Manispaa hiyo.
Amesema tayari Serikali Kuu imetoa kiasi fedha za Kitanzania Billion Saba (Tsh 7,000,000,000/=) kwa ajili ya ujenzi wa Soko hilo ambalo litakuwa na maduka 250 na Ujenzi wa eneo la Wajasiriamali zaidi ya 1000.
Amesema tayari Mkandarasi amekabidhiwa eneo la ujenzi huku akisema soko hilo litajengwa kwa Kuta za kubwa za kuzuia maji ya ziwa (Gabions) ukilinganisha na Soko lililokuwepo awali lililoathiriwa na maji.
Amesema ujenzi huo unaenda sambamba na Ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha lami katika eneo hilo.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa