Na Mwandishi Wetu
Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya kigoma/Ujiji mapema Leo Januari 22, 2026 wamepata mafunzo ya kidijitali ya mfumo wa ofisi mtandao (e-office management System) yaliyofanyikia katika ukumbi wa Manispaa hiyo.
Mafunzo hayo yameongozwa na Wataalamu kutoka Ofisi ya Rais idara ya kumbukumbu na nyaraka yakihudhuriwa na Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na Watumishi wa Makao makuu ya Ofisi ya Mkurugenzi.
Akiwasilisha katika mafunzo hayo Afisa Kumbukumbu kutoka Ofisi ya Rais idara ya Kumbukumbu na nyaraka Ndugu. Godwin Nyange amesema Mfumo wa E-Office unalenga kupunguza gharama na kurahisisha Mawasiliano na kukabiliana na Changamoto ya kuhifadhi nyaraka.
Amesema Mfumo huo unarahisisha mzunguko wa majalada ndani ya taasisi za Umma, na kufanya maamuzi sahihi kwa wakati.
Katika Mafunzo hayo Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu Ndugu. David Rwazo amewashukuru kwa mafunzo hayo huku akisema Mfumo wa E-Office utaanza kutumika hivi karibuni baada ya Mafunzo kukamilika kwa Watumishi.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa