Na Mwandishi Wetu
Halmashauri ya Manispaa ya kigoma/Ujiji Jana Desemba 02, 2025 ilikabidhi pikipiki Sita (06) kwa vikundi viwili (02) vya Wajasiriamali ikiwa ni Mkopo wa 10% kwa Makundi ya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu.
Pikipiki hizo zilikabidhiwa kwa kikundi cha Hapa kazi kilichopo Kata ya Mwanga kaskazini na Kikundi cha Watu wenye Ulemavu kilichopo Kata ya Majengo zikiwa na gharama ya Tsh 21,514,000/= kwa Kushirikiana na Bank ya CRDB.
Akitoa taarifa katika makabidhiano hayo Mratibu wa Mikopo Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Jabir Majira alisema katika awamu hii ya pili ya utoaji mikopo jumla ya vikundi 58 vimenufaika na mkopo usiokuwa na riba wa fedha za Kitanzania zaidi ya Million Mia Tano (Tsh 555,652,400/=).
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa