Na Mwandishi Wetu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameahidi Serikali kuleta fedha kwa ajili ya ujenzi wa kisasa wa mabanda ya Soko la Kibirizi lililopo Manispaa ya Kigoma/Ujiji
Amesema hayo Leo October 18, 2022 wakati akihutubia Wananchi wa waliojitokeza katika eneo la soko la Kibirizi mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika Ujenzi wa bandari ndogo ya Kibirizi
Rais amesema kutokana na maboresho ya Bandari yanayoendelea Serikali italeta fedha ili mabanda yaliyopo soko la kibirizi yajengwe kisasa kwa lengo la kuboresha mazingira ya Wafanyabiashara wa soko hilo waliopo jirani na bandari hiyo
Aidha amewataka wafanyibiashara waliopo katika soko hilo kukubaliana na maboresho hayo kwa kupisha ujenzi huo pindi fedha zitakapokuwa tayari na Halmashauri kuweka utaratibu wa kuwapa kipaumbele wafanyabiashara hao watakaopisha mara baada ya ujenzi kukamilika
Amesema “ ni lazima Wafanyabiashara mkubaliane tufanye ujenzi wa Kisasa, tufanye ramani mpya ya soko , Mkubaliane na ubomoaji ili kuboresha mazingira yenu ya kazi”
Katika bandari ya kibirizi iliyowekwa jiwe la Msingi jumla ya fedha za Kitanzania Billion 32/= zinatumika katika ujenzi unaoendelea katika bandari ya Kibirizi na Ujiji ikihusisha ujenzi wa Jengo la abiria, Jengo la Mizigo na ujenzi wa gati
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa