Na Mwandishi Wetu
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassani amesema Serikali imepanga ujenzi wa hospitali ya kanda ya Magharibi Mkoani Kigoma itakayohudumia Wakazi wa Mkoa huo na mikoa jirani kama vile Tabora na Katavi
Ameyasema hayo alipokuwa akihutubia Wananchi mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika ujenzi unaoendelea Hospali ya Rufaa Mkoa wa Kigoma (Maweni) kwa ujenzi wa Jengo la Wagonjwa Mahututi (ICU) na jengo la magonjwa ya dharura ukigharimu kiasi cha fedha za Kitanzia Billion 1.3 na uwekaji wa vifaa tiba kwa gharama ya kiasi fedha za Kitanzania Billion 1.5
Amesema Serikali kuu imepanga kuleta fedha za Kitanzania Billion 5 kwa lengo la Ujenzi wa Hospitali ya Kanda ya Magharibi ili kuepusha Wananchi wa kanda hiyo kufuata huduma ya matibabu ya Kibingwa mbali kama vile Hospitali ya Bugando na Mhimbili
Amesema kutokana na kutokamilika kwa ujenzi wa jengo la Wagonjwa mahututi (ICU) katika hospitali hiyo ya Maweni Serikali itaongeza fedha za Kitanzania Billion 2 ili kukamilisha ujenzi katika jengo hilo
Aidha amesema katika Hospitali hiyo baadhi ya huduma kama vile siti scan zinatarajia kuanza Mwezi Novemba Mwaka huu huku akiwataka Watumishi wa afya kuendelea kufanya kazi kwa uaminifu
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa