Na Mwandishi Wetu
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Ndugu. Hassan Rugwa Leo May 13, 2024 amefanya ziara ya kukagua ujenzi unaoendelea katika Hospitali ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Kiongozi huyo amefanya ziara ya kukagua majengo yanayoendelea kujengwa kama vile jengo la Maabara, Jengo la Wazazi (Maternity Complex), Jengo la mionzi, na jengo la stoo ya dawa.
Katibu Tawala huyo ameutaka uongozi wa Manispaa kuendelea kusimamia kasi ya Ujenzi wa Majengo hayo ili kukamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa Wananchi.
Serikali ya Awamu ya Sita ilileta fedha za Kitanzania Billion Moja na Million Mia tatu (Tsh 1, 300, 000, 000/=) kwa ajili ya Ujenzi wa Majengo hayo ikiwemo Jengo la Wagonjwa wa nje (OPD) ambalo tayari linafanya kazi ikiwemo Mapumziko ya mda mfupi na vipimo vya maabara.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Mwantum Mgonja amemhakikishia Kiongozi huyo kusimamia maelekezo aliyoyatoa ikiwemo kusimamia miundombinu kukamilika kwa wakati.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa