Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Idara ya mipango na Uchumi Ndugu. Julius Ndele Jana January 14, 2025 aliwasilisha rasimu ya mpango na bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka wa fedha 2025/2026 katika kikao cha kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) iliyofanyika katika Ukumbi wa Kigoma Social hall.
Kikao hicho kiliongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dr. Rashid Chuachua Kikihudhuriwa na Meya wa Manispaa Mhe. Baraka Naibuha Lupoli, Waheshimiwa Madiwani, Wakuu wa Idara na Vitengo, Viongozi wa vyama vya siasa na Wakuu wa taasisi mbalimbali.
Akiwasilisha katika kikao alitaja vipaumbele vinavyotarajiwa kutekelezwa katika bajeti hiyo ikiwa ni pamoja na kukuza ukusanyaji wa mapato ya ndani na kuboresha huduma za jamii, Ukamilishaji wa miradi viporo, Utekelezaji wa Sheria za kisekta, Kuongeza ufanisi katika kushughulikia masuala mtambuka, kusimamia usafi wa Mji na uhifadhi wa Mazingira.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa