Jumla ya kaya 503,762 zinatarajiwa kunufaika na mpango wa ugawaji wa vyandarua 1,775,359 vilivyotolewa na Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Afya ikiwa ni utekelezaji Mpango wa Taifa wa kudhibiti Maralia (NMCP) ambapo Mkoa wa Kigoma ni miongoni mwa mikoa yenye kiwango kikubwa cha maambukizi.
Akizindua rasmi zoezi la ugawaji wa vyandarua hivyo kupitia hafla fupi iliyofanyika katika Zahanati
ya Mtaa wa Rusimbi Manispaa ya Kigoma Ujiji, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amesema kwa mujibu wa taarifa zinazotolewa kupitia mfumo wa kutolea taarifa za wagonjwa (TDHS), kwa mwaka 2024 jumla ya wagonjwa 309,080 walibainika na maambukizi ya ugonjwa huo kimkoa, ambapo idadi ya vifo ilikuwa watu 264 vikihusisha watoto 177 na watu wazima 87.
Amesema vyandarua hivyo vinatolewa bure na serikali hivyo wasimamizi wanapaswa kusimamia vizuri zoezi la ugawaji ili viwafikie walengwa huku akitoa wito kwa wanufaika kufanya matumizi sahihi ili viweze kuleta tija katika kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa maralia mkoani Kigoma na nchini kwa ujumla.
Aidha amewataka walengwa ambao watanufaika na mpango huo katika halmashauri zote nane za mkoa, kuvitumia vyandarua hivyo kwa usahihi na kuachana na dhana potofu kuwa matumizi yake yanaweza kuchangia kupunguza nguvu za kiume au kusababisha changamoto za uzazi kwa wanawake.
Naye Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Hassan Rugwa amesema zoezi la ugawaji wa vyandarua hivyo litazigusa kaya zote ndani ya mkoa wa Kigoma.
Amesema wakazi wameendelea kuwa mashuhuda kwa ā°kujionea namna serikali ya awamu ya sita inavyoendelea kuwagusa wananchi kupitia uboreshaji mkubwa katika utoaji wa huduma za Afya nchini.
Victor Sungusia, Afisa Ugavi MSD amewataka wananchi kutumia vyandarua hivyo kwa lengo la kujikinga na maralia ili kutumia muda wao katika kufanya kazi za maendeleo badala ya kushinda wakishuhulikia changamoto za kiafya zitokanazo na maradhi hayo.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa