Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro Leo OKtoba 15, 2025 amefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi inayotekelezwa Manispaa ya Kigoma/Ujiji kupitia Mradi wa uboreshaji wa miundombinu ya Miji kiushindani Tanzania (TACTICS).
Mkuu huyo wa Mkoa amefanya ziara na kukagua ujenzi unaoendelea wa daraja la Mto Ruiche, Ujenzi wa kiwango cha lami Barabara ya Bangwe-Ujiji yenye urefu km 7, Ujenzi wa soko la Mwanga, Ujenzi Korongo la katonyanga, Burega,Bushabani na mfereji wa kutoa maji Katubuka.
Akiwa katika miradi amepongeza namna ujenzi unavyoendelea huku akimtaka Mkandarasi mjenzi kuhakisha anafanya kazi kwa weredi na kwa wakati.
Meneja wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu.Eliasi Mtapima amesema ujenzi wa Barabara na mitalo ya maji unatarajia kukamilika Mwezi Februari 2026 .
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa