Na Mwandishi Wetu
Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dr. Samia Suluhu Hassan imeendelea na uboreshaji upatikanaji wa huduma za matibabu katika kituo cha afya cha Gungu kilichopo Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa ununuzi wa vifaa tiba vyenye thamani ya fedha za Kitanzania zaidi ya Million Mia tatu (Tsh 300, 000, 000/=)
Huduma za matibabu kwa wagonjwa wa nje zimeendelea kutolewa ikiwa ni pamoja na huduma ya upasuaji iliyozinduliwa mapema mwezi January , 2023 ambapo hadi sasa zaidi ya Wanawake sitini na nane (68) tayari wamepatiwa huduma hiyo
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kigomà /Ujiji Dr. Hashim Mvogogo anasema Serikali imefanikisha ujenzi wa jengo la Wagonjwa wa Nje, Maabara, Jengo la kufulia, Jengo la wodi ya Wazazi na Upasuaji katika kituo hicho cha afya cha Gungu kwa gharama ya fedha za Kitanzania Millioni Mia tano (Tsh 500, 000, 000/=) ikiwa ni pamoja na ununuzi wa vifaa vya Upasuaji pamoja na vifaa vya uhifadhi damu salama
Serikali imeendelea kuboresha upatikanaji wa vifaa katika kituo hicho cha afya ambapo zaidi ya Fedha za Kitanzania Million mia tatu (Tsh 300, 000, 000/=) zimetolewa na Serikali kuu kwa ajili ununuzi wa vifaa tiba kama Mashine ya Usingizi, Kitanda cha upasuaji, Ununuzi wa taa jengo la upasuaji, Mashine ya kutakasia vifaa na friji ya kuhifadhia damu
Uboreshaji na upatikanaji wa huduma katika kituo hicho ikiwa ni pamoja na upasuaji na kuongeza damu kumeondoa utoaji rufaa kwa Wagonjwa kuelekea katika hospitali ya Babtisti na Hospitali ya rufaa ya Maweni
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa