Na Mwandishi Wetu
Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji Jana May 04, 2025 ilipokea mahitaji ya Chakula na vifaa vya msaada wa kibinadamu kwa Wananchi Walioathirika na maji ya Mvua kutoka Serikali Kuu chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu).
Serikali imetoa msaada huo wa kibinadamu kwa kutoa Chakula cha msaada Mahindi Tani 15,648, Maharage Kg 4,694, Godoro 283, Blanketi 283, ndoo 283, na mikeka 283.
Mahitaji hayo ya msaada wa kibinadamu yatagawiwa kwa waathirika kutoka katika Kata ya Katubuka, Kibirizi, Buzebazeba na Bangwe.
Ofisi ya Waziri Mkuu imetoa pole kwa waathirika wote kutokana na kadhia ziliwapata Wananchi katika maeneo yao.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa