Na mwandishi wetu
Mkuu wa wilaya ya Buhigwe Luteni Kanal Micheal Masala Nganyalina leo march 6, katika uwanja wa Lake Tanganyika uliopo manispaa ya Kigoma/ ujiji asema serikali itaendelea kuwachukulia hatua waharifu na wanaosababisha uharifu katika kuhafifisha ufaulu kwa watoto wa kike kwa kuwatumikisha na kuwafanyia vitendo vya uharifu.
Ameyasema hayo alipokuwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo iliandaliwa na idara ya elimu Manispaa ya KIgoma /Ujiji kutokana na kuendelea kuona ufaulu kwa watoto wa kike kuendelea kuwa mbaya kuanzia mwaka 2014 hadi matokeo ya mwaka wa 2018.
Akizungumzia taarifa iliyotolewa na Kaimu afisa elimu msingi Ndugu. Kisinga(kwa jina moja) ya kuporomoka kwa ufaulu wa wanafunzi wa kike Manispaa ya Kigoma/Ujiji amesema hali ni mbaya ukilinganisha na ufaulu wa watoto wa kike na kusema ni lazma wataalamu wa elimu kukaa na kuhakikisha wanafunzi wa kike matokeo yao yanakuwa juu ukilinganisha na matokeo yaliyopita ya darasa la saba ambapo kwa mwaka 2014 walifaulu kwa asilimia 18.6 na kuzidi kuporomoka ambapo kwa mwaka 2018 wanafunzi wa kike wamefaulu kwa asilimia 10.9 ukilinganisha na wanafunzi wa kiume.
Katika sherehe hizo Mstahiki Meya wa manispaa ya Kigoma/Ujiji Mhe. Hussein Ruhava akitoa nasaha zake amewataka wanasiasa kkuhubiri katika majukwaa wanafunzi wa kike kupata fursa sawa kama wanafunzi wa kiume na kuachana na masuala ya kuwatumikisha kazi za nyumbani pamoja na masoko ya usiku.
Ameendelea kusema kwa sasa wanafunzi wa kike wasiogope kwenda shule hata wanapokuwa katika siku zao kwani nguo za kujisitiri tayari zinapatikana mashuleni, vyumba vya kujikagua mashuleni na uwepo wa walimu wa ushauri nasaha katika kila shule.
Naye kaimu Mkurugenzi wa manispaa Ndugu. Brown Nziku amesema tayari bajeti imepangwa kwa ajili ya kukuza miundombinu na mazingira ya kujifunza kwa wanafunzi wa kike na serikali inaendelea kujenga miundombinu kuhakikikisha wanafunzi waliokosa nafasi za kujiunga na kidato cha kwanza wanapata nafasi ya kuendelea na masomo hasa katika sekondari inayojengwa kata ya Buzebazeba.
Katika sherehe hiyo iliambatana na burudani mbalimbali nyimbo na maigizo kutoka kwa wanafunzi pamoja na kuleta viongozi mbalimbali wa kike na kuzungumza na wanafunzi katika kuleta hamasa kwa wanafunzi wa kike ili waweze kufikia malengo yao.
PICHA ZA TUKIO HUSIKA INGIA KATIKA MAKTABA YA PICHA.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa