Baraza la madiwani wa halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji jana Novemba 15, limepitisha hoja ya kutunga sheria ndogo ya kudhibiti ngono zembe kutokana na kuongezeka kwa vitendo vya biashara ya ngono katika manispaa hiyo
Hoja hiyo iliyoibuliwa na diwani wa kata ya Kibirizi Mhe Yunus Rohomvya baada ya mjumbe wa kamati ya UKIMWI Mhe. Obadia Manwigi kuwasilisilisha taarifa ya robo ya nne katika baraza hilo ambapo alisema kumekuwa na ongezeko kubwa la mabinti wa eneo la Kibirizi,Bangwe, na Ujiji kila siku za jioni kwenda mjini na eneo la Community Centre maarufu kwa Bera kukusanyika eneo hilo ili waweze kukutana na wanaume kwa lengo la kujiingizia kipato
Akieendelea kutoa hoja hiyo alisema hata hivyo kuna kundi kubwa la mabinti kutoka Nchi jirani ya Burundi wanafanya biashara katika maeneo mbalimbali ya starehe katika manispaa hiyo, baada ya kutoa taarifa hiyo diwani huyo aliwataka madiwani wa halmashauri hiyo kuunga mkono hoja kwa kukubaliana na wazo la kutunga sheria ndogo hiyo
Aidha awali mjumbe wa kamati ya Ukimwi akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo alisema kwa kipindi ha robo ya nne kiwango cha watu kuugua magonjwa ya ngono zembe yameongezeka ukilinganisha na kipindi kilichopita ambapo wagonjwa 544 walipimwa na kukutwa na magonjwa hayo wabaume wakiwa 76 na wanawake wakiwa 468
Nao baadhi ya madiwani wakichangia hoja hiyo wamekubaliana na hoja hiyo kutokana na vitendo hivyo kukithiri katika manispaa hiyo akichangia hoja hiyo Diwani viti maalumu Mhe Stella alisema ‘vitendo hivyo ni vibaya vinavyoendelea katika mji wetu tunapaswa kutovifumbia macho kutokana na athari zinazoweza kujitokeza katika mji wetu ikiwa na kupoteza nguvu kazi za vijana wetu’
Aidha Baraza hilo limeweza kutoa pongezi kwa halmashauri ya manispaa ya kigoma/Ujiji kwa kuongeza kiwango cha ufaulu katika matokeo ya mtihani wa kitaifa wa darasa la saba kwa mwaka 2019 na kuibuka mshindi wa kwanza katika halmashauri nane za mkoa wa Kigoma
Baraza hilo limetoa vinyago kwa shule tatu zilizofanya vibaya na kuwa wa mwisho katika mtiririko wa mshindi kwa shule za halmashauri hiyo , shule zilizofanya vibaya ni pamoja na shule ya msingi Businde, shule ya msingi Mbano na shule ya msingi Benjamini Mkapa.
Mwenyekiti wa kamati ya Uchumi,Elimu na Afya Mhe. Hussein Kaliyango alisema kamati imeweka mikakati ya kuhakikisha manispaa hiyo inaendelea kufanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi na elimu ya Sekondari ambapo amesema kamati zote za shule zimeshaitwa na kukabidhiwa mikakati hiyo.
Akiendelea kueleza alisema mikakati hiyo ni pamoja na kila shule kuhakikisha inapata kompyuta na printa kwa ajili ya kufanya mitihani na majaribio kila mara na kuhakikisha kamati za shule zinasimamia kupungua kwa utoro kwa shule zilizopo katika manispaa hiyo.
Naye mkurugenzi wa halmashauri hiyo Ndugu. Mwailwa Pangani alisema kufikia mwezio Desemba manispaa hiyo itahakikisha inanua tofali laki moja na elfu sitini na tano(165,000) na kila shule iliyopo katika manispaa hiyo itapata tofali elfu ishirini na tano(25,000).
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa