Na Mwandishi Wetu
Wajumbe wa kamati ya lishe Sekta mtambuka Manispaa ya Kigoma/Ujiji wamekutana Leo Septemba 30, 2025 kwa lengo la kujadili utekelezaji wa afua za lishe.
Katika kikao hicho Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Kigoma Ujiji Bi. Ephata Msiga amewasilisha Utekelezaji wa Programu jumuishi ya Kitaifa ya malezi, makuzi na maendeleo ya Watoto.
Amesema katika kulinda afya ya Watoto Wataalamu wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa kipindi cha Januari-Julai wamefikia Kaya 685 zenye Watoto 2973 katika Kata 19 na kutoa elimu na kupima hali ya lishe kwa familia zenye Wajawazito na Watoto chini ya miaka mitano ili kukinga na kutibu utapiamlo.
Amesema tayari Manispaa ya Kigoma/Ujiji imepokea mashine mbili (02) za kuongeza Virutubisho ambapo Wasindikaji wa unga wamepatiwa mafunzo ya kuongeza Virutubisho kwenye unga wa mahindi.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa