Na Mwandishi Wetu
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Ndugu. Hassan Rugwa amewataka Wananchi na wakazi wa Mkoa wa Kigoma kujitokeza kupata huduma za matibabu ya Kibingwa kwa awamu ya nne katika kambi za Madaktari bingwa na Madaktari bobezi.
Ameyasema hayo Leo Septemba 29,2025 katika ukumbi wa Jengo la Mkuu wa Mkoa wa Kigoma alipokuwa akizindua kuanza kwa Utoaji wa huduma za matibabu ya Kibingwa katika Halmashauri za Mkoa.
Aidha amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo ameendelea kusogeza huduma za matibabu ya kibingwa Karibu na Wananchi na kuwafikia Watu wengi kwa gharama nafuu.
Mganga Mkuu wa Mkoa Dr. Damas Kayera amesema Mkoa wa Kigoma umepokea Madaktari arobaini na nane (48) ambao watahudumia Wananchi na kuwajengea uwezo Watumishi wa Kada ya afya katika Halmashauri zote nane (08) za Mkoa wa Kigoma kwa mda wa siku Saba (07) kuanzia Septemba 29 hadi Oktoba 03, Mwaka huu.
Amesema katika Awamu tatu za Matibabu zilizopita Wananchi na wakazi wa Mkoa wa Kigoma 7,605 walipata huduma za Matibabu ya Kibingwa huku Wananchi 380 wakipata huduma za upasuaji na Watumishi 288 walijengewa uwezo katika Utoaji huduma.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa