Na Mwandishi Wetu
Mafunzo ya uandaaji na utengenezaji wa zana za kufundishia na kujifunzia kwa Walimu wa darasa la kwanza na la pili yanaendelea Shule ya Msingi Kigoma.
Mafunzo hayo yanayofadhiliwa na Mradi wa Shule Bora yalianza Jumatatu Desemba 1, 2025 ikiwa ni Siku ya tatu (03) tangu kuanza yakitolewa na Wataalamu kutoka Tanzania Teachers Workshop.
Mshiriki wa Mafunzo hayo kutoka Shule ya Msingi Mugunga Mwalimu Mohammed Athumani anasema mafunzo yanawajengea uwezo wa uandaaji wa zana za kufundishia na kujifunzia na zitazowesha kurahisisha ujifunzaji wa Mwanafunzi kutumia Milango yote ya fahamu katika Kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK).
Mradi wa Shule Bora umeendelea kuwezesha Walimu kuboresha mbinu za ufundishaji na ujifunzaji kwa kutoa mafunzo, Mradi huu ni Programu ya elimu inayofadhiliwa na Serikali ya Uingereza ikilenga kuboresha elimu katika Shule za Serikali kwa ngazi ya elimu awali na msingi kwa kuongeza ubora, Ujumuishi na Usalama.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa