Na Mwandishi Wetu
Shule Mpya ya awali na Msingi katika Kata ya Buhanda inarajiwa kuwa matumaini katika kufikia ndoto ya elimu kwa Wanafunzi wa Mtaa wa Mgeo Kata ya Buhanda Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa kupunguza kutembea umbali mrefu.
Ujenzi wa miundombinu umefikia asilimia tisini na nane (98%) ambapo kwa sasa ukamilishaji wa madawati, viti na meza ukiwa unaendelea.
Wanafunzi wanatarajia kuanza masomo yao hivi karibuni katika Shule hiyo wakigawanywa kutoka Shule Mama (Shule ya Msingi Mwasenga na Butunga) za Kata hiyo.
Kwa sasa Wanafunzi wa Mtaa wa Mgeo wanatembea Wastani wa Km 3 kwenda Shule ya Msingi Mwasenga na Butunga ambapo kuanza kwa masomo katika Shule hiyo kutafanya Wanafunzi kutembea Wastani wa Km 1 kwenda Shuleni hapo.
Serikali ya Awamu ya Sita imetekeleza ujenzi wa Shule hiyo Mpya kupitia Mradi wa BOOST ili kusogeza huduma, kuepuka wanafunzi kutembea umbali mrefu na kupunguza wingi wa Wanafunzi madarasani.
Ujenzi wa Shule ya Awali na Msingi unatekelezwa kwa gharama ya fedha za Kitanzania zaidi ya Million Mia tatu (Tsh 342,900,000/=).
Uenzi huu unahusisha jengo la Utawala, Vyumba vya madarasa viwili (02) vya elimu ya Awali, Vyumba Sita (06) elimu Msingi, Madawati , Viti, Meza na Matundu ya Vyoo kumi na nane(18).
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa