Na Mwandishi wetu
Shule ya Msingi Mgumile iliyopo kata ya Kagera Manispaa ya Kigoma/Ujiji imezingirwa na maji ya ziwa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha mwanzoni mwa mwezi marchi na kufanya Manispaa hiyo kuanza na ujenzi wa madarasa ya mda
Akizungumza Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndugu Mwailwa Pangani alipokuwa akikagua hatua za ujenzi na ukamilishaji wa madarasa hayo ya mda amesema maji hayo yalizingira shule baada ya likizo iliyotangazwa nchini kutokana na Mlipuko wa Ugonjwa wa Corona hali ambayo mwanzoni walidhani maji yangepungua na kuisha miundombinu ikiwa salama
Ameendelea kusema maji yaliyojaa katika eneo hilo la shule limesababisha madarasa na nyumba za walimu kujaa maji suala lililoleta usumbufu kwa walimu kuacha Makazi hayo na kutafuta makazi mengine huku miundombinu ya majengo ikisalia kuwa katikati ya maji
Mkurugenzi huyo amesema tayari hatua za awali zimechukuliwa kutokana na maji hayo kutopungua ambapo madarasa ya mda nane (8) yamejengwa , Ofisi moja (1) ya walimu pamoja na vyoo vya walimu na wanafunzi vilivyogharimu kiasi cha Fedha Milion ishirini na mbili (Tsh 22,000,000/=) katika eneo alilolitoa mwananchi huku nguvu ya wananchi ikitumika katika kuhamisha madawati na vitabu kutoka shule ya awali
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo ameishukuru Serikali kwa hatua za haraka za ujenzi wa miundombinu ya shule kwa haraka na kwa wakati huku akisema vipindi vya masomo tayari vimeanza kwa baadhi ya madarasa na hapo kesho wanampango wa kuendelea na ratiba kama ilivyo kuwa imepangwa
Naye mmoja wa wananchi aliyetoa ardhi ya hekari 4 Ndugu Mangereka Ramadhani amesema ametoa ardhi hiyo ili wanafunzi waendelee na masomo yao kama ilivyo kuwa awali na changamoto waliyokumbana nayo ya kukaa likizo ya mda mrefu iliyotokana na ugonjwa wa Corona
Ameendelea kusema katika kutoa ardhi ni pamoja na kuunga Juhudi za Serikali ambapo imeboresha na kujenga miundombinu mbali mbali ya Afya, na Elimu Nchini ikiwa ni katika kuboresha mazingira ya wananchi Wanyonge
Naye mmoja wa Wananchi Bi. Marry Hassan ameishukuru Serikali kwa kujenga miundombinu
ya haraka ili Kunusuru kupotea kwa vipindi vya wanafunzi katika ujifunzaji, na kusema changamoto ya kujaa maji imeleta athari kubwa sana kwa miundombinu ya serikali hata baadhi ya Makazi ya Wananchi Kuvunjika huku akiitaka serikali kuja na mkakati wa kujenga madarasa ya kudumu tofauti na eneo la awali la shule hiyo
Picha zaidi ingia maktaba ya picha www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa