Na Mwandishi Wetu
Manispaa ya Kigoma/Ujiji imepokea kiasi cha fedha za Kitanzania zaidi ya Billioni mbili na Millioni Mia tano (Tsh 2,504,597,857.00/=) Kutoka Serikali Kuu kupitia Mradi wa BOOST kwa ajili ya Ujenzi wa miundombinu ya elimu ya awali na Msingi.
Fedha hizo zinatarajia kujenga Shule Mpya za Awali na Msingi nne (04) zenye Mkondo mmoja katika Kata za Kagera eneo la Mgumile, Kibirizi eneo la Buronge, Buhanda na Businde Kila Shule ikigharimu kiasi cha fedha za Kitanzania zaidi ya Million Mia tatu arobaini na mbili (Tsh 342, 900,000/=).
Pia fedha hizo zinalenga Kukarabati Shule Kongwe ikiwemo Shule ya Msingi Kagera kwa gharama ya Tsh 111, 197, 857/= na ukarabati wa Shule ya Msingi Ujiji kwa gharama ya Tsh 151,000,000/=.
Aidha ujenzi wa miundombinu ya madarasa na Matundu ya vyoo yanatarajia kujengwa katika Shule ya Msingi Bushabani, Rasini, Kagera, Kitongoni, Kipampa, Burega, Uhuru na Shule ya Msingi Mwenge.
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dr. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia ili watoto wa Kitanzania wapate elimu bora katika mazingira rafiki na salama.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa