Na Mwandishi Wetu
Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani yakiambatana na maadhimisho ya Wiki ya Chanjo Kitaifa yamefanyika ngazi ya Mkoa Leo April 26, 2025 katika kituo cha afya cha Ujiji Manispaa ya Kigoma.
Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Mgeni Rasmi Afisa Tawala Wilaya ya Kigoma Bi. Dorah Buzaile kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Viongozi na Wananchi wa Manispaa hiyo.
Akiwasilisha taarifa katika maadhimisho hayo Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Dr. Hashim Mvogogo amesema Serikali imetoa vyandarua 1,040,000 vyenye thamani ya fedha za Kitanzania Billion 3/= na tayari Kaya 48,208 sawa na 96% kati ya Kaya 50,090 zimeandikishwa ili kupata vyandarua na Lita 2200 zinatarajia kutumika ili kupulizia maeneo yenye mazalia ya Mbu.
Chanjo inatarajia kutolewa kwa Watoto walio chini ya umri wa miaka 5 kwa mda wa Siku 7 katika Vituo vyote vya kutolea huduma za afya.
Katika Uzinduzi huo Mgeni rasmi ametoa Chakula dawa kwa Watoto waliotambuliwa kuwa kuwa na utapiamlo kwa kugawa kopo za maziwa lishe 500 na Karanga lishe zenye thamani ya Millioni Moja na Laki nane (Tsh 1,800,000/=) kutoka Mapato ya ndani.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa