Na Mwandishi Wetu
Ujenzi wa mfereji wa kutoa maji ya mvua Kata ya Katubuka kuelekea ziwani wenye Km 3.3 umeanza kutekelezwa kwa gharama ya fedha za Kitanzania Billion nne na millioni mia tisa (Billion 4.9/=).
Jana Septemba 09, 2025 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma IGP (Mst). Mhe. Balozi Simon Sirro alifanya Mkutano wa hadhara na Wananchi wa Kata ya Katubuka kwa lengo la kuwajulisha namna Serikali ambavyo inaendelea kushughulikia kuweka miundombinu kudumu ya kuondoa maji ya mvua katika eneo hilo.
Naibu Waziri wa OR-TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba (Mb) ambaye alihudhuria Mkutano huo alisema Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kuboresha miundombinu rafiki na Salama kwa Wananchi huku akimtaka Mkandarasi wa Ujenzi kufanya kazi kwa weredi na kwa mda uliopangwa.
Ujenzi wa mfereji huo wa maji ulionza unatekelezwa kwa kipindi cha miezi mitatu ambapo utakamilika mwezi Novemba Mwaka huu huku Mkandarasi wa ujenzi ikiwa ni Kampuni ya CRJE.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa