Na Mwandishi Wetu
Timu ya Wataalamu kutoka Ofisi ya Rais Tawala ya Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wamefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya awamu ya kwanza inayoendelea kutekelezwa kupitia mradi wa uboreshaji wa miji kiushindani Nchini Tanzania (TACTICS) Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Ziara hiyo imefanyika Leo July 11, 2024 ambapo wamekagua na kutoa ushauri kwa mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi kwa kuongeza Wataalamu na vifaa vya kazi ili kuendana na wakati.
Aidha wameitaka Halmashauri kuendelea kushirikiana na taasisi zingine ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza na kuathiri wananchi ikiwemo miundombinu ya maji na umeme pamoja na kuratibu na kutatua malalamiko ya Wananchi kwa wakati.
Mradi unaoendelea kutekelezwa wa Awamu ya kwanza ni pamoja na Ujenzi wa Barabara ya Wafipa-Kagera yenye urefu wa Km 2.434, Daraja la Mto Ruiche, Ujenzi wa barabara ya Bangwe-Burega- Ujiji yenye urefu wa Km 7.01, na Ujenzi wa mitaro ya kutiririsha maji ya Mvua katika maeneo ya Bangwe Km 0.687, Burega Km 1.040, Rutale Km 1.263, Mlole Km 0.468 , Bushabani Km 0.581 , Mji mwema Km 0.888, na mfereji wa maji Katonyanga yenye urefu Km 0.483 kwa gharama ya fedha za Kitanzania zaidi ya Billion ishirini na tisa ( Tsh 29,813,388,456.50/=) kwa mda wa Miezi kumi na tano.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa