Na Mwandishi Wetu
Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa ya Watu na Makazi Wilaya ya Kigoma ambaye ndiye Mkuu wa Wilaya hiyo Bi. Ester Alexander Mahawe amewataka wajumbe wa kamati hiyo ngazi ya Wilaya kuendelea kutoa elimu ya Ushiriki wa Wananchi katika zoezi hilo linalotarajia kufanyika Agosti 23, 2022
Ameyasema hayo leo June 2, 2022 katika kikao cha kwanza cha kamati hiyo kilichofanyikia Kigoma Social hall huku akiwataka wajumbe kutoa elimu na kusimamia kamati zilizoundwa ngazi ya kata, Mitaa na vitongoji ili kuhakikisha elimu inawafikia Wananchi na wakazi kushiriki Sensa kikamilifu
Amesema umuhimu wa Sensa ya Watu na Makazi kwa Watanzania ni pamoja na Serikali kupata taarifa za msingi zitakazosaidia mchakato wa Utekelezaji wa dira ya Maendeleo ya Mwaka 2025, mageuzi ya masuala ya afya na jamii, pamoja na ufuatiliaji wa ajenda za maendeleo kitaifa na kimataifa
Ameendelea kusema umuhimu mwingine ni pamoja na Serikali kujua na kupata takwimu ya Ongezeko la idadi ya watu itakayosaidia katika upangaji bajeti na Maendeleo kwa Wananchi
Mratibu wa Sensa ya Watu na Makazi Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Frednand Filimbi amesema kamati hiyo imeshaanza utoaji wa elimu kupitia vyombo vya habari, Tovuti za Serikali, Mitandao ya Kijamii na elimu itaendelea kupitia mikutano ya Wananchi, Taasisi za dini na makundi mbalimbali ili kuwafikia Wananchi wengi
Aidha kikao hicho kimejadili Majukumu ya wajumbe, kupitia Miongozo ya kazi, na kujadili maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi 2022
#sensayawatunamakazi2022 #sensa2022 #jiandaekuhesabiwa
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa