Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ndugu. Salum Hamisi Kali amewataka maafisa elimu kata Manispaa ya Kigoma/Ujiji kusimamia suala la ufundishaji na ujifunzaji kwa lengo la kuendelea kukuza elimu na viwango vya ufaulu Shuleni
Ameyasema hayo Leo February 16, 2023 alipofanya kikao na maafisa elimu ngazi ya Kata katika ukumbi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji
Mkuu huyo wa Wilaya amewataka kusimamia na kudhibiti utoro kwa kufanya vikao na kamati za Shule kwa kushirikiana na Wenyeviti wa Serikali za mitaa na kubaini Wanafunzi ambao wanashindwa kuhudhuria masomo na kuhakikisha Wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na masomo ya upili wanaripoti kabla ya March 01, mwaka huu
Aidha amewataka maafisa elimu hao kusimamia miradi inayoendelea kujengwa kwa kuhakikisha thamani ya miradi na fedha iliyopangwa vinaendana
Awali Afisa Elimu Msingi Ndugu. Richard Mtauka kwa niaba ya Afisa elimu Sekondari amesema Wanafunzi 5574 sawa na asilimia 92 wameanza masomo huku ambao hawajaripoti wakiendelea kufuatiliwa na maafisa elimu ngazi ya kata wakishirikiana na viongozi ngazi ya mtaa
Naye Afisa elimu kata ya Rusimbi Ndugu. Lilenga Issaya amemhakikishia Mkuu huyo wa Wilaya kufanya kazi kwa pamoja kwa kushirikiana na Viongozi wa elimu hata kuwashirikisha katika mikutano ya kitaaluma kwa lengo la kuinua ufaulu na viwango vya elimu kwa shule za Msingi na Sekondari
Mkuu huyo wa Wilaya amekuwa akikutana na makundi mbalimbali ya wadau wa maendeleo kwa lengo la kupanga na kuweka mikakati katika sekta mbalimbali na ameahidi kufanya ziara Shuleni kwa kufanya vikao na Walimu pamoja na Wanafunzi kwa lengo la kukuza viwango vya elimu
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa