Na Mwandishi Wetu
Katibu Tawala Msaidizi Serikali za Mitaa Mkoani Kigoma Ndugu. Moses Msuluzya amewataka Wananchi wa Wilaya ya Kigoma kudumisha amani iliyopo Nchini Tanzania
Ameyasema hayo Leo Desemba 9, 2022 katika Kongamano la miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania bara awali ikiitwa Tanganyika liloandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kigoma likifanyikia Ukumbi wa NNSF Kigoma
Amesema Wananchi wa Wilaya ya Kigoma na Watanzania wote kila mmoja ana wajibu wa kuhakikisha analinda amani iliyoasisiwa na Viongozi wa Taifa hilo pasipo kuruhusu vurugu ya aina yeyote
Aidha amewataka Wananchi hao kutumia fursa zilizopo Mkoani Kigoma kama kilimo cha Michikichi ya Kisasa, Uvuvi, biashara na kutumia mipaka ya Nchi jirani katika kujiongezea kipato na kukuza Uchumi
Amewataka Wakuu wa taasisi, Idara na Vitengo Serikalini kuendelea kutoa taarifa kwa Wananchi juu ya miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Wilaya hiyo katika kuboresha huduma za jamii
Katika kongamano hilo Wakuu wa taasisi wameeleza mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 61 tangu uhuru wa Tanganyika awali ikiitwa Tanganyika kabla ya kuungana na Zanzibar Mwaka 1964 na Kuuitwa Tanzania
Kongamano hilo limehudhuliwa na Barozì mdogo wa Burundi Nchini Tanzania, Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Kigoma, Wakurugenzi wa Taasisi, Wakuu wa idara, Viongozi wa Kisiasa, Wananchi na Wandishi wa habari
Kauli mbiu ya Mwaka huu ni " Miaka 61 ya Uhuru, Amani na Umoja ni nguzo ya Maendeleo yetu ".
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa