Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dr. Rashid Chuachua amewataka Wakuu wa Idara na Maafisa Watendaji wa Kata kuendelea kuelimisha suala la lishe ili kuepuka udumavu katika jamii.
Ameyasema hayo Leo July 22, 2025 wakati akifungua kikao cha tathimini ya Utekelezaji wa afua za lishe kwa kipindi cha April-June 2024/2025 Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Amewataka Watendaji Kata kusimamia majiko darasa kwa Jamii na Wanafunzi ili kuwa na uwezo wa kuandaa chakula kwa kuzingatia mlo kamili.
Aidha amewataka kuendelelea kusimamia kilimo kwa Shule zenye ardhi ili kupata mazao ya nafaka na matunda kwa ajili ya Chakula kipindi cha masomo.
Afisa Lishe Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Omary Kibwana amesema Halmashauri imeendelea kuazimisha siku ya afya na lishe ngazi ya Mtaa kwa kutoa elimu ya uandaaji wa lishe Bora , na uhamasisha elimu ya lishe kupitia vyombo vya habari na Mikutano ya Wananchi.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa