Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Kisena Mabuba amewataka Wananchi wa Manispaa hiyo kuendelea kujivunia mji huo kutokana na ukuaji wa Kiuchumi na utekelezaji wa miradi mikubwa ya Masoko inayoendelea.
Amesema ujenzi wa kisasa Soko la Mwanga unaendelea ambapo litakuwa na uwezo wa kuchukua Wafanyabiashara zaidi ya 2000, sambamba na Ujenzi wa Soko la Mwalo wa Katango na Ujenzi wa Soko la Kibirizi unaoanza ukigharimu zaidi ya fedha za Kitanzania Billion 7 .
Amewataka Wananchi kuendelea kuwekeza katika Sekta ya kibiashara kutokana na mazingira wezeshi ambayo Serikali imeendelea kuboresha.
www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa