Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Kisena Mabuba Leo Februari 10, 2024 amempokea Kamishina wa Tume ya Haki za binadamu na misingi ya Utawala Bora Mhe. Amina Talib Ali.
Kamishina akiwa Ofisi ya Mkurugenzi amesema amekuja na Wataalamu mbalimbali kwa lengo la kutoa elimu kwa Umma kuhusiana na haki za binadamu pamoja na misingi ya utawala bora.
Amesema tume hiyo itatoa elimu kwa Watendaji na Watumishi wa Serikali na kuzungumza na Wananchi katika maeneo yao ili kuona namna haki za binadamu na misingi ya utawala bora inavyotekelezwa.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa