Na Mwandishi Wetu
Chama cha Ushirika cha Ubumwe Carpental Cooperative Limited Jana Oktoba 15, 2025 kimetoa Madawati kumi (10) kwa Shule ya Msingi Ujiji iliyopo Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Madawati hayo yenye thamani ya fedha za Kitanzania Million moja na laki tano (Tsh 1,500,000/=) yametolewa na Chama hicho cha Ushirika ikiwa ni takwa la Kisheria kwa taasisi mbalimbali kutoa michango ya maendeleo ndani ya jamii (Corporate Social Responsibility - CSR).
Akizungumza mara baada ya kukabidhi Madawati hayo Mnajisi Msaidizi wa vyama vya ushirika Mkoa wa Kigoma Ndugu. Richard Damian Majalla aliitaka Jamii kuunga juhudi za vyama vya ushirika ili kuendelea kutoa michango mbalimbali katika Jamii.
Aidha aliwataka Wanafunzi kuendelea kutunza miundombinu ili kuwawezesha katika suala la ujifunzaji na kukuza taaluma zao.
Mwenyekiti wa bodi ya chama cha Ushirika cha Ubumwe Carpental cooperative limited Ndugu. Sekunda Ndabhiyegese aliwataka Wakazi wa Mkoa wa Kigoma kuendelea kuwaunga Mkono kwa kununua samani bora wanazozizalisha kutokana na kuwa na mafundi Seremala walio mahiri.
Mratibu Elimu Kata wa Kata ya Kipampa Bi.Fortunata Mpantwa mara baada ya kupokea Madawati hayo alikipongeza chama hicho cha Ushirika huku akisema miundombinu hiyo itaboresha ujifunzaji na ufundishaji kwa Wanafunzi na Walimu.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa