Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Ndugu. Thobias Adengenye Jana Julai 03, 2023 aliwataka Wakuu wa Wilaya kusimamia vikao vya kila robo vya tathimini ya lishe ili kuweza kuendelea kuondoa hali ya udumavu kwa Watoto
Aliyasema hayo katika kikao cha tathimini ya lishe kwa Mkoa kilichofanyikia ukumbi wa Katibu Tawala wa Mkoa huo kikihusisha Katibu Tawala wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Waganga Wakuu, Maaifisa lishe, Wakuu wa Mipango, na Wakuu wa idara ya Fedha kutoka Sekritarieti ya Mkoa na Halmashauri
Katika hotuba Aliyoitoa alisema kwa kipindi cha Miaka mitatu Mkoa wa Kigoma umepunguza hali ya udumavu kutoka asilimia 42 hadi asilimia 27 kwa hali ilivyo kwa sasa
Alisema katika kuondoa udumavu lazima elimu iendelee kutolewa kuanzia ngazi ya familia wakiwemo Wanaume jambo litakalosabisha ukuaji wa uzalishaji Mali pamoja na kukua kwa uchumi katika Mkoa wa Kigoma
Naye Katibu Tawala wa Mkoa Ndugu. Albert Msovera aliwataka Maafisa lishe kukagua chumvi zinazouzwa katika minada kama zinakidhi viwango na kuwa na madini Joto kwa afya ya walaji
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa