Mkuu wa wilaya ya Kigoma Ndugu Samson Anga leo may 16 amezitaka kamati tisa za malalamiko za mradi wa uendeshaji miji ya kimkakati Tanzania Strategic Cities Project(TSCP) kutoa mafunzo kwa wananchi katika utunzaji na kubaini waharibifu wa miundombinu iliyopo na inayoendelea kujengwa.
Ameyasema hayo katika ufunguzi wa semina ya kamati za malalamiko iliyoendeshwa katika ukumbi wa mkutano just in time chini ya wawezeshaji Zainabu Ngonyani na Beatrice Mchoma kutoka Ofisi ya Raisi wizara ya tawala za mikoa na serikali za mitaa(TAMISEMI)
Amesema zipo kata ambazo zina wananchi ambao ni waharibifu wa miundombinu kama wizi wa sola na taa za barabara katika barabara ya mwasenga, dampo la taka msiba jambo ambalo linahafifisha kupendeza kwa mji na hata kuhafifisha maendeleo ya kata husika.
Mkuu wa wilaya ametaka kamati hizo katika utekelezaji wa majukumu yao ya kupokea malalamiko katika ujenzi wa miundombinu pia kuhakikisha kutoa elimu kwa kuwajulisha wananchi maendeleo hayo ni kwa manufaa yao lakini pia kamati hizo zisaidie katika kubaini wezi hao na waharibifu kwa lengo la kuwafikisha katika vyombo vya sharia.
Semina hiyo chini ya wawezeshaji kutoka wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) wametoa semina hiyo kwa kueleza majukumu ya kamati hizo ikiwa ni kusikiliza malalamiko ya wananchi, kuitafautia ufumbuzi kwa viongozi wa halmashauri kama Mkurugenzi na kutoa mrejesho kwa walalamikaji(wananchi) katika ujenzi wa miundo mbinu mbalimbali kwa miradi inayosimamiwa na TSCP chini ya ufadhili wa Benki ya dunia.
Aidha wawezeshaji hao wameshukuru Benki ya dunia katika miradi iliyokwisha tekelezwa chini ya Tanzania Strategic Cities Project(TSCP) wameibanisha ambayo ni ujenzi wa stendi za mabasi kama vile stendi kuu ya mkoa Masanga, stendi ya Kigoma mjini na ujenzi wa stendi ya Kasingirima, ambapo miradi mingine iliyokwisha tekelezwa ni pamoja na mifereji ya kupitisha maji eneo la Rubengera, NHC Katubuka, ujenzi wa barabara ya Rusimbi kwa kiwango cha lami, ujenzi wa dampo la kisasa msiba, na ujenzi wa ofisi za kukatia tiketi stendi kuu ya mabasi Masanga. Ambapo miradi ambayo inayotarajiwa kutekelezwa ni ujenzi wa barabara ya Nazarethi , barabara ya kagashe, barabara ya Burega na barabara ya Mwembetogwa.
Zainabu Ngonyani ambaye alikuwa mwezeshaji katika semina hiyo amesema katika kusikia na kutatua malalamiko wana kamati hao lazima wawe wastaarabu, waweze kushirikisha wataalamu kutoka ngazi ya manispaa katika kutatua malalamiko na malalamiko hayo ya wananchi kuweza kutatuliwa kwa wakati na walalamikaji kupata mrejesho.
Ameendelea kusema kamati wanaweza kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusiana aidha vumbi, kelele na kutolipwa kwa fidia wakati wa ujenzi wa miundombinu kama vile barabara na mifereji ya kupitishia maji ya mvua, watu wengine wanaoweza kulalamika ni wanasiasa, taasisi kama vile makanisa na msikiti, watawala na hata watumishi wa halmashauri husika.
Amesema kamati za malalamiko lazima kufanya kazi kwa ufanisi ili kuepuka vyanzo vya malalamiko ambavyo ni kushindwa kufuata utaratibu katika ujenzi wa miundombinu na ukosefu wa taarifa kwa wananchi.
Semina hiyo iliyohudhuliwa na mkurugenzi wa halmashauri ya Kigoma/Ujiji Dr.John Shauri Tlatlaa naye pia amewataka wanakamati kuwa tayari katika kupokea malalamiko ya wananchi na kuzifanyia kazi kwa wakati ikiwa ni kuziwasilisha kwa wataalamu husika wa halmshauri ambapo amewataka pia watendaji wa kata kutenga ofsi kwa ajili ya malalamiko ya wananchi ikiwa ni pamoja na kutambulisha kamati hizo kwa wananchi wa kata husika kata ya mwanga kusini imefanya vizuri katika utekelezaji huo,
Mkurugenzi ameendelea kusema miradi hiyo inapojengwa italeta ajira kwa wakazi na wananchi wa manispaa na kuwataka wanakamati hao kufanya kazi kwa ufanisi.
Aidha baahi ya wajumbe wa kamati hizo za malalamiko waliohudhulia mafunzo hayo bwana Hamza Haji kutoka kata ya Machinjioni na mhe. Rugomoka kutoka kata ya katubuka wameshukuru wawezeshaji hao kwa kusema watatoa ushirikiano mzuri katika kushugulikia malalamiko na kuyafikisha kwa wataalamu kwa wakati na kusema mabadiliko makubwa ya kimaendeleo yanatarajiwa katika manispaa kwa miradi iliyokamilika na inayotarajiwa kujengwa.
Semina hiyo imejumuisha wawezeshaji kutoka katika TAMISEMI, mkuu wa wilaya ya Kigoma, mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya kigoma ujiji, na wanakamati kutoka katika kata tisa ambazo ni kata ya Rusimbi, kata ya Mwanga kusini, kata ya Mwanga kaskazini, kata ya Kigoma, kata ya katubuka,kata ya kitongoni, kata ya Buzebazeba, kata ya kagera, ambapo wawezeshaji hao wamemaliza semina hizo mchana na kuelekea mkoani Mwanza kwa lengo la mafunzo kama hayo.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa