Na Mwandishi Wetu
Ujenzi wa mfereji ya maji ya mvua wenye urefu wa Km 3.52 unaendelea kutekelezwa Kata ya Katubuka Manispaa ya Kigoma/Ujiji kupitia Mradi wa uboreshaji wa miji na majiji kiushindani (TACTICS).
Ujenzi huu unatekelezwa na Kampuni ya CRJE (East Africa Limited) kwa gharama ya fedha za Kitanzania Billioni tano (Tsh Billion 5.7/=) ikiwa ni kazi ya nyongeza katika mradi wa awamu ya Kwanza (Package I) ambao ni Ujenzi wa Barabara ya Bangwe -Ujiji, Ujenzi wa Daraja la Mto Ruiche pamoja na mifereji ya maji ya Mvua.
kukamilika kwa ujenzi wa mfereji Katubuka kutafanya maji yaliyotuama kwenda ziwani na kuondoa adha ya uhalibifu wa miundombinu na makazi ya Wananchi wa Kata hiyo.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa