Na Mwandishi Wetu
Ujenzi wa Shule Mpya ya awali na msingi yenye Mkondo mmoja Kata ya Businde Manispaa ya Kigoma/Ujiji unaendelea.
Serikali inatekeleza Ujenzi huu kupitia Mradi wa BOOST kwa gharama ya fedha za Kitanzania zaidi ya Million Mia tatu (Tsh 342,900,000/=).
Ujenzi huu unahusisha jengo la Utawala, Vyumba vya madarasa viwili (02) vya elimu ya Awali, Vyumba Sita (06) elimu Msingi, Madawati , Viti, Meza na Matundu ya Vyoo kumi na nane(18).
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dr. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha Mazingira ya Utoaji elimu kwa Wananchi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji ili kuhakikisha wahitimu wanakuwa wenye maarifa na Ujuzi stahiki.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz @mabuba_fkm @rashid_chuachua @samia_suluhu_hassan @msemajimkuuwaserikali
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa