Na Mwandishi Wetu
Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuboresha Mazingira ya Utoaji elimu kwa Wananchi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji ili kuhakikisha wahitimu wanakuwa wenye maarifa na Ujuzi stahiki.
Serikali imeanza kutekeleza ujenzi wa Shule ya Awali na Msingi mpya katika Kata ya Businde iliyopo Manispaa ya Kigoma/Ujiji kupitia Mradi wa BOOST kwa gharama ya fedha za Kitanzania zaidi ya Million Mia tatu (Tsh 342,900,000/=).
Aidha ujenzi huu unahusisha jengo la Utawala, Vyumba vya madarasa viwili (02) vya elimu ya Awali, Vyumba Sita (06) elimu Msingi, Madawati , Viti, Meza na Matundu ya Vyoo kumi na nane(18).
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa