Na Mwandishi Wetu
Michoro ya ujenzi wa soko la Kibirizi kisasa Jana February 10, 2023 iliwasilishwa Kwa Wakuu wa idara na Vitengo,wakiwa na Viongozi wa Wafanyabiashara wa soko hilo
Uwasilishaji huo ulifanyika katika Ukumbi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji na Wataalamu na Wahandisi kutoka mamlaka ya Bandari (TPA) mara baada ya kufanya upembuzi wa awali
Mhandisi kutoka Mamlaka ya Bandari (TPA) Makao makuu Eng. Twaha Msita awali akiwasilisha Mwonekano wa michoro ya Ujenzi wa soko hilo alisema awali ziara ilifanyika katika soko hilo kwa lengo la kutambua ukubwa wa eneo na kujua gharama za vifaa vya ujenzi katika Manispaa ya Kigoma/Ujiji
Aliwasilisha michoro itakayojengwa katika Soko hilo ikiwa ni pamoja na michoro ya Ujenzi wa Shedi za Wafanyabiashara wa mazao ya uvuvi, Mabanda, michoro ya Ujenzi wa Migahawa ya vyakula, michoro ya ujenzi wa vituo vya kupaki daladala, Bajaji na boda boda
Mhandisi kutoka Mamlaka ya Bandari (TPA) Eng. Hamis Mbutu aliwataka Wataalamu, Viongozi wa Wafanyabiashara, Wafanyabiashara pamoja na Wananchi kuendelea kutoa maoni juu ya Ujenzi wa soko hilo na kujengwa kulingana mahitaji ya Watumiaji wa soko hilo
Aidha katika kikao hicho, Wataalamu na Viongozi wa Wafanyabiashara walitoa maoni na mapendekezo ya awali, huku akisema maoni mengine yataendelea kukusanywa kwa Wadau kama Vile Wafanyabiashara, Wananchi pamoja na Viongozi wa Kisiasa na Serikali
Itakumbukwa pia ujenzi wa soko hilo kisasa ni ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan aliyoitoa October 18, 2022 akiwahutubia wananchi wa eneo la Kibirizi mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika Ujenzi wa bandari ndogo eneo la Kibirizi
Rais alisema kutokana na maboresho ya Bandari yanayoendelea Serikali italeta fedha ili mabanda yaliyopo soko la kibirizi yajengwe kisasa kwa lengo la kuboresha mazingira ya Wafanyabiashara wa soko hilo waliopo jirani na bandari hiyo
Ujenzi wa soko hilo la Kibirizi kisasa utawanufaisha Wafanyabiashara soko kuwa na Miundombinu ya Kisasa, Uwepo wa mifumo ya Ulinzi na Usalama, kukua kwa biashara ya Wafanyabiashara, na Halmashauri katika ukusanyaji wa Mapato
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa