Na Mwandishi Wetu
Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji imeanza ujenzi wa Zahanati mpya katika Kata ya Rubuga kupitia Mapato ya ndani kwa lengo la kuendelea kusogeza huduma za matibabu karibu na Wananchi.
Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji tayari imeshatoa kiasi cha fedha za Kitanzania Million Mia moja (Tsh 100, 000,000/=) kutoka katika Mapato ya ndani ujenzi ukiwa Katika hatua ya msingi, na kukamilika kwa jengo kunatarajia kutumia kiasi cha fedha za Kitanzania Millioni Mia moja thelathini ( Tsh 130,000,0000/=).
Ujenzi huu umeanza kwa kuwanufaisha Wakazi wa Kata hiyo katika hatua ya ujenzi kwa kujipatia vipato kupitia mafundi ujenzi, Vibarua, mama lishe, Madereva wa malori na boda boda.
kukamilika kwa ujenzi wa Zahanati hiyo kutawanufaisha Wananchi wa Kata hiyo na maeneo jirani ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Ibara ya 81 katika kuhakikisha Serikali inatoa huduma za afya na Wananchi kuwa na afya bora ili kuwawezesha kushiriki Shuguli za Maendeleo Nchini.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa